1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yakubali kurefusha makubaliano ya ngano

17 Mei 2023

Rais Reccep Tayyip Erdogan wa Uturuki amesema Urusi imekubali kurefusha makubaliano ya kusafirisha nafaka za Ukraine kupitia Bahari Nyeusi hadi sehemu zinazokabiliwa na njaa duniani kwa kipindi cha miezi miwili.

https://p.dw.com/p/4RVsr
Ukraine | Das Getreideterminal im Hafen von Odessa
Picha: Bo Amstrup/Ritzau Scanpix/picture alliance

Hatua hii ni afueni kwa usalama wa chakula duniani baada ya vita vya Ukraine vilivyoanza zaidi ya mwaka mmoja uliopita kusababisha ongezeko la bei za vyakula.

Urusi ilikuwa imeweka Alhamis (Mei 18) kuwa muda wa mwisho kwa maslahi yake kuzingatiwa la sivyo ijiondoe kutoka kwenye makubaliano hayo yaliyosimamiwa na Uturuki na Umoja wa Mataifa.

Kuongezwa kwa makubaliano hayo ni hatua muhimu kwa nchi za Afrika, Mashariki ya Kati na baadhi ya sehemu za Asia ambazo zinategemea nafaka, mafuta na bidhaa za vyakula vya bei rahisi kutoka Ukraine.