Urusi yaelekeza nguvu kudhibiti Mashariki mwa Ukraine
11 Agosti 2022Mamalaka katika eneo la Dnipropetrovsk imethibitisha watu watatu kuuwawa na wengine saba kujeruhiwa kwa makombora katika mji wa Nikopol wakati roketi 120 ziliposhambulia eneo hilo na kuongeza kuwa vikosi vya Urusi vimeelekeza nguvu za mashambulizi ili kutwaa udhibiti kamili wa maeneo muhimu ya mashariki mwa Ukraine la Luhask na Dionetsk.
Mapigano makali yamezuka karibu na mji wa mashariki wa Pisky leo Alhamis huku mataifa ya Magharibi na Ukraine yakivishutumu vikosi vya Urusi kwa kutumia mitambo ya nyuklia katika kuzuwia mashambulizi ya mizinga.
Soma zaidi:Rais Zelensky asifu mafanikio ya jeshi la Ukraine
Msemaji wa jeshi la Ukraine Oleskandar Shtupun amesema, bado kuna tishio la mashambulizi ya makombora dhidi ya vifaa vya kijeshi pamoja na miundombinu muhimu na kuhimiza kila mmoja kutopuuza tahadhari za mashambulizi ya anga.
"Adui ameelekeza nguvu zote katika kudhibiti mikoa ya Luhansk na Donesk."
Aliongeza kwamba kuendeleza udhibiti katika mkoa unaokaliwa kwa muda wa Khersonna sehemu za mikoa ya Mykolaiv na Zaporizhzhia kunatoa mwelekeo mwingine katika mapamabano hayo.
"Hilo linatoa mazingira rafiki kwa ajili ya kuanzianzisha upya mashambulizi katika maeneo tofauti na kuzuia mawasiliano ya Ukraine kupitia bahari nyausi" Alisema Oleksandr
Ukraine yakanusha Donetsk kuwa chini ya Urusi
Afisa wa Jamhuri ya Donetsk inayounga mkono vikosi vya Urusi amekaririwa na vyombo vya habari akisema kwamba mji mkuu wa mkoa wa Donetsk, Pisky, ulikuwa chini ya udhibiti wa Urusi na vikosi vinavyotaka kujitenga.
Ukraine imekanusha mji huoambao ni ngome ya ulinzi katika eneo hilo na Donetsk kuwa upo chini ya udhibiti wa Urusi.
Kanda ya Donbas, inayojumuisha mikoa ya Luhansk na Donetsk ni shabaha muhimu kwa vikosi vya Urusi nchini Ukraine baada ya kushindwa kutwaa udhibiti wa mji mkuu Kyiv mwanzoni kabisa mwa vita mnamo mwezi Februari.
Soma zaidi:Mashambulizi dhidi ya kinu cha nyuklia cha Zaporizhzhya yaongeza wasiwasi
Kwa sasa mapambano makali yanashuhidiwa katika ardhi ya Donetsk kati ya vikosi vya Urusi na Ukraine wote wakiwania udhibiti wa eneo hilo la kimkakati.
Picha za Satilaiti zilizotolewa leo zimeonesha uharibifu katika kambi ya anga ya Urusi huko Crimea, baada ya mripuko wa siku ya Jumanne ambao Urusi inasema ulikuwa tukio la ajali, lakini wadadisi wanashuku ulitokana na mashambulizi ya Ukraine, japokuwa taifa hilo pia limesalia kimya kuhusu hilo.