Urusi na China zafanya luteka za pamoja za kijeshi
21 Julai 2023Wizara ya ulinzi ya Urusi, imesema lengo mahususi la luteka hizo zinazohusisha ndege 30 za majeshi ya wanamaji na zitakazofanyika hadi Jumapili ni kuimarisha ushirikiano wa majeshi yao ya majini na kudumisha utulivu na amani katika ukanda wa Asia-Pasifiki.
Soma pia: Urusi na China zasaini mikataba ya kiuchumi
Luteka hizo zitahusisha makabiliano ya majini na baharini na hewani, wizara hiyo imesema na kuongeza kuwa kuna mipango pia ya kufanya luteka za pamoja za ufyatuaji wa mizinga.
Katika hatua nyingine, Urusi imefanya mazoezi ya kijeshi kaskazinimagharibi mwa Bahari Nyeusi, wizara hiyo imesema hii leo, siku chache baada ya ikulu ya Kremlin kusema kuwa itazingatia meli zinazokwenda Ukraine kupitia njia hiyo ya baharini kuwa kiticho cha kijeshi.