SiasaUrusi
Urusi na China zakosoa tamko la mwisho la mkutano wa G7
20 Mei 2023Matangazo
Waziri wa mambo ya kigeni wa Urusi Sergei Lavorv amesema maamuzi yaliyofikiwa na kundi la G7 yanalenga "kuzidhibiti" Urusi na China kwa kutumia mzozo wa Ukraine kama silaha ya kufanya hivo.
Lavrov alikuwa akizungumzia dhamira iliyoelezwa na kundi la G7 ya kuendelea kuipatia silaha Ukraine na kuongeza mbinyo kwa Moscow kupitia vikwazo vya kiuchumi kuilazimisha isitishe vita nchini Ukraine.
Kwa upande wake, China imesema haijaridhishwa hata kidogo na tamko la mwisho la mkutano wa Hiroshima ikiwemo ukosoaji juu ya kujitanua kwake kijeshi kwenye bahari ya kusini mwa China na rikodi yake dhaifu ya haki za binadamu.
China imesema mataifa ya G7 yameutumia mkutano huo kuipaka matope nchi hiyo na kuingilia masuala yake ya ndani.