1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUfaransa

Bunge la Ulaya lamrejesha Ursula von der Leyen

18 Julai 2024

Bunge la Ulaya limemchagua tena Ursula von der Leyen kuhudumu kwa muhula wa pili kama Rais wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya kwa kura 401.

https://p.dw.com/p/4iTUv
Strassbourg 2024 | Von der Leyen | Uchaguzi wa Halmashauri Kuu ya Ulaya
Ursula von der Leyen akionyesha furaha baada ya kuchaguliwa kwa muhula wa pili kuongoza Halmashauri ya Umoja wa UlayaPicha: Johannes Simon/Getty Images

Von der Leyen amepata kura 401, wabunge 284 walimpinga na wengine 15 hawakuwepo. Kura saba zikiharibika.

Mnamo mwaka 2019, alichaguliwa kwa wingi wa kura tisa pekee, japo wakati huu tofauti ya wingi wa kura alizozipata ni zaidi ya 40.

Katika hotuba yake bungeni kabla ya kupiga kura, von der Leyen aliahidi kuchukua hatua ili kuuinua uchumi wa Ulaya, kuimarisha usalama na kutetea demokrasia.

Kuchaguliwa tena kwa von der Leyen kuongoza moja ya taasisi zenye nguvu barani Ulaya kwa miaka mitano mingine, ni ishara ya utulivu ndani ya Umoja wa Ulaya wakati inapopitia nyakati ngumu za vita na kuongezeka kwa siasa kali za mrengo wa kulia.