SiasaZimbabwe
Upinzani Zimbabwe waitisha maandamano kupinga uchaguzi
1 Septemba 2023Matangazo
Mwito huo kutoka kwa chama cha Citizens Coalition for Change (CCC) umetolewa siku moja baada ya Mnangagwa kusema uchaguzi ulikuwa halali, huku akionya yoyote atakayesababisha ghasia atachukuliwa hatua kali.
Maandamano hayo yatafanyika katika majimbo 10 ya Zimbabwe , huku chama hicho kikiwaomba wanaharakati kuanzisha kampeni za mitandaoni na kusambaza ushahidi wa udanganyifu uliofanyikwa kwenye uchaguzi huo. CCC kina siku saba za kuwasilisha madai ya kupinga matokeo hayo ya uchaguzi mahakamani, tangu tume ilipotangaza rasmi.
Tume ya taifa ya uchaguzi ya Zimbabwe ilimtangaza Mnangagwa kushinda uchaguzi kwa asilimia karibu 53 na mpinzani wake Nelson Chamisa wa CCC akipata asilimia 44.