Upinzani nchini Zimbabwe wataka uchaguzi urudiwe tena
29 Agosti 2023Matangazo
Chama kikuu cha upinzani nchini Zimbabwe cha Citizens' Coalition for Change (CCC) kimetaka uchaguzi ufanyike upya baada ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa wiki iliyopita ambao chama hicho kilisema ulikabibiiwa na udanganyifu.
Naibu msemaji wa chama cha CCC, Gift Siziba amewambia waandishi wa Habari kwamba chama hicho kilikuwa kikitoa wito kwa Umoja wa Afrika na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC, kuwezesha kurejesha hali ya kufuata sheria na kanuni katika nchi hiyo ya kusini mwa Afrika.
Tume ya uchaguzi ya Zimbabwe mwishoni mwa wiki iliyiopita ilimtangaza Rais aliyemaliza muda wake Emmerson Mnangagwa wa chama tawala cha ZANU-PF kuwa ndiye mshindi wa kura ya urais lakini wachambuzi wamehoji uhalali wa matokeo hayo.