1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaVenezuela

Upinzani wawataka Wavenezuela kumpinga Maduro

1 Agosti 2024

Kiongozi wa upinzani nchini Venezuela Maria Corina Machado amewatolea wito wafuasi wake kuungana baada ya Rais Nicolas Maduro kuapa kusalia madarakani kufuatia uchaguzi unaozozaniwa.

https://p.dw.com/p/4izZ8
Maandamano ya kupinga matokeo ya uchaguzi Venezuela
Licha ya maandamano makubwa, Rais Nicolas Maduro ameapa kusalia madarakani kufuatia uchaguzi tataPicha: Mika Otsuki/AP/picture alliance

Machado ametoa ujumbe huo katikati ya sintofahamu kubwa nchini humo, baada yaMaduro kutangazwa kushinda uchaguzi wa Jumapili, lakini mamlaka za uchaguzi zikishindwa kutoa matokeo kwa kina juu ya ushindi huo.

Machado ameandika kwenye mtandao wa X, akiwaomba wafuasi kuungana dhidi ya matokeo hayo kwa sababu wanaufahamu ukweli.

Marekani, Brazil na Umoja wa Ulaya wamezishinikiza mamlaka za nchi hiyo kuchapisha takwimu kamili, wakati White House ikionya kwamba muda wa uvumilivu wa jamii ya kimataifa, unazidi kuyoyoma.