Maduro atangazwa mshindi katika matokeo ya uchaguzi wa rais
29 Julai 2024Matokeo hayo yametangazwa usiku wa kuamkia leo.
Hata hivyo upinzani unajiandaa kuyapinga matokeo hayo na huenda hatua hiyo ikaitumbukiza Venezuela katika hatari ya kuingia kwenye mkwamo mkubwa wa kisiasa.
Mamilioni ya raia wa taifa hilo walitegemea uchaguzi huo kuwa nafasi pekee ya kuumaliza utawala wa miaka 25 wa chama kimoja. Serikali nyingi ikiwemo ya Marekani zimejizuia kuutambuwa ushindi wa Maduro.
Soma pia: Marekani na Venezuela zabadilishana wafungwa
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken amesema nchi yake ina mashaka makubwa na matokeo yaliyotangazwa, ikiwa yanaakisi kweli matakwa ya wananchi.
Rais wa Chile Gabriel Boric amesema utawala wa Maduro unapaswa kutambuwa kwamba matokeo iliyoyachapishwa ni vugumu kuaminika.
Rais Vladmir Putin wa Urusi amempongeza Maduro kwa kuchaguliwa tena.