Upinzani wapinga matokeo ya uchaguzi Zimbabwe
28 Agosti 2023Chamisa anayeongoza muungano wa upinzani wa Citizens Coalition for Change (CCC) alisema wameshinda uchaguzi huo na wana viongozi, akiongeza kuwa walishangazwa kusikia Mnangagwa akitangazwa mshindi.
Kulingana na Tume ya Uchaguzi ya Zimbabwe (ZEC), Mnangagwa ameshinda kwa asilimia 52.6 akimuangusha mpinzani wake wa karibu, Chamisa, aliyetangazwa kupata asilimia 44.
Soma zaidi: SADC: Uchaguzi Zimbabwe haujakidhi mahitaji ya katiba
Matokeo ya kwanza ya majimbo yatolewa Zimbabwe
Mapema, Mnangagwa aliwataka wanaoyapinga matokeo hayo kwenda mahakamani.
Waangalizi kutoka Umoja wa Ulaya na Jumuiya ya Madola na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) walielezea mashaka yao kwenye mchakato mzima wa uchaguzi huo tangu kwenye kuzuiwa kwa mikutano ya wapinzani, uandikishwaji wa wapiga kura, upendeleo wa vyombo vya habari hadi kutishwa kwa wapigakura.