1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaVenezuela

Upinzani Venezuela kuandamana kupinga matokeo ya uchaguzi

2 Agosti 2024

Kiongozi wa upinzani nchini Venezuela Maria Corina Machado ameitisha maandamano hapo kesho Jumamosi katika kila mji nchini humo kupinga kuchaguliwa kwa mara nyengine kwa Rais wa Venezuela Nicolas Maduro.

https://p.dw.com/p/4j1q1
Venezuela | Uchaguzi wa rais nchini Venezuela
Kiongozi wa upinzani wa Venezuela Maria Corina Machado akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uchaguzi wa urais, huko Caracas, Venezuela Julai 29, 2024.Picha: Leonardo Fernandez Viloria/REUTERS

Machado amerudia kauli yake kwamba mgombea wa upinzani Edmundo Gonzalez Urrutia ndiye mshindi halali akisema alishinda kwa asilimia 67 dhidi ya 30 za Maduro, kutokana na hesabu iliyofanywa katika vituo vingi vya kura kote nchini humo. Marekani na Umoja wa Ulaya wamezitaka mamlaka za Venezuela kutoa data kamili zauchaguzi huo, huku waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Antony Blinken akisema kuna "ushahidi wa kutosha" unaoonesha kwamba Gonzalez ndiye aliyeshinda uchaguzi. Uchaguzi huo wa Jumapili venezuela ulifanyika chini ya kiwingu cha onyo la Maduro kwamba kutakuwepo na "umwagikaji damu" endapo angeshindwa. Machado anasema karibu watu 20 wamefariki dunia kutokana na maandamano yaliyozuka baada ya uchaguzi huo.