Upinzani utakata rufaa kupinga urais wa Tinubu Nigeria
7 Septemba 2023Wagombea wakuu wa upinzani katika nafasi ya urais wa Nigeria kupitia wanasheria wao wamesema watakata rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama uliothibitisha ushindi wa rais Bola Tinubu katika uchaguzi wa urais wa mwezi Februari ambao ulikuwa na utata.
Soma pia: Mahakama Nigeria kuamua kuhusu ushindi wa Tinubu
Wagombea Atiku Abubakar wa chama cha People's Democratic Party na Peter Obi wa Labour Party's ambao walishika nafasi ya pili na yatatu kwenye uchaguzi huo, waliwasilisha mahakamani kesi ya kutaka uchaguzi ufutwe kwa madai ya wizi wa kura na mawakala kushindwa kuchapisha matokeo ya uchaguzi kupitia mtandao.
Soma pia: Rais wa Nigeria akabidhiwa mikoba ya ECOWAS
Lakini Mahakama ya rufaa ya Nigeria hapo jana ilitupilia mbali maombi yao katika hukumu ambayo iliyosomwa kwa zaidi ya saa 11.
Wakili wa Obi, Livy Uzoukwu, aliwaambia wanahabari kuwa timu yake itaipitia hukumu kikamilifu na kukata rufaa katika Mahakama ya Juu.
Soma: Bola Tinubu aapishwa kuwa Rais wa Nigeria
Rufaa katika Mahakama ya Juu nchini humo, inapaswa kuwasilishwa ndani ya 14 siku kutoka tarehe ya uamuzi wa mahakama na Mahakama Kuu ina siku 60 za kusikiliza kesi hiyo na kutoa uamuzi wake.