1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN:Watoto milioni 7 wameathirika kote Uturuki na Syria

14 Februari 2023

Umoja wa Mataifa umesema zaidi ya watoto milioni 7 wameathirika kwa tetemeko la ardhi nchini Uturuki na Syria, yaliyotokea wiki iliyopita.

https://p.dw.com/p/4NTT0
Erdbebenkatastrophe in der Türkei
Picha: Bulent Kilic/AFP

Bado kuna wasiwasi mkubwa kuwa maelfu  kwa maelfu ya watoto huenda wakawa wameuwawa katika janga hilo. 

James Elder, msemaji wa shirika la Umoja huo la kuwahudumia watoto, UNICEF, amesema nchini Uturuki pekee idadi jumla ya watoto walioathirika katika mikoa 10 iliyokumbwa na matetemeko hayo mawili ya ardhi ilifikia milioni 4.6. huku Syria ikiwa na watoto milioni 2.5 walioathirika na hali hiyo. 

Soma pia:Waokoaji waendelea kufukua waliokwama Uturuki na Syria

Ameyasema hayo wakati timu ya uokozi ikijianda kukamilisha operesheni zake za kuwatafuta manusura wa janga hilo lililosababisha vifo vya watu zaidi ya elfu35,000 katika mataifa yote mawili.