Uganda:Mmoja afariki kwa tetemeko Uturuki
14 Februari 2023Ubalozi wa nchi hiyo umetoa taarifa hiyo huku ukiwahimiza raia wake na wa mataifa mengine ya Afrika Mashariki kuwasiliana na maafisa wake wapate misaada midogo ya dharura na hususani kuwezeshwa kuwasiliana na jamaa zao.
Kufuatia juhudi zinazoendelea Uturuki za kufukua vifusi kuwasaka watu waliokwama baada ya tetemeko la ardhi, raia mmoja mwanamke wa Uganda amepatikana akiwa alifariki.
Hicho ndicho kifo cha kwanza ambacho kimeripotiwa rasmi na balozi wa Uganda nchini Uturuki, Nusura Tiperu.
Soma pia:Waokoaji waendelea kufukua waliokwama Uturuki na Syria
Maiti ya raia huyo kwa jina Florence Babirye ilipatikana katika vifusi mkoa wa Hatay, moja kati ya sehemu zilizoathirika zaidi.
"Ubalozi umethibitisha wanafunzi wawili waathirika,mmoja amefariki." Alisema balozi wa Uganda Uturuki.
Ubalozi waUganda umeendelea kuwatafuta raia wake walioko Uturuki kufahamu hali zao na kuwawezesha jamaa zao kuwasiliana nao.
Hadi sasa kati ya raia 16 walioweza kuwasiliana na ubalozi huo, mmoja ambaye alipata majeraha anaendelea kupata matibabu katika hospitali moja mji mkuu wa Malatya.
Wengi wapata wasiwasi juu ya kjamaa zao
Jamaa na marafiki wa raia walioko Uturuki wameendelea kufuatilia taarifa hizo kwa makini na baadhi yao wangali katika mashaka makubwa kuhusu hali za jamaa zao ambao hawajaweza kuwasiliana nao tangu kutokea kwa tetemeko hilo lilipotokea tarehe 6 mwezi huu.
Wanasema wanatamani kufahamu juu ya ndugu na jamaa zaoa ambao walikumbwa na mkasa huo juma lililopita.
"Tunahitaji kujua juu ya ndugu zetu" Alisema mwanamke mmoja alipozu ngumza na DW.
Balozi Nusura Tiperu amewahimiza raia wa mataifa mengine ya Afrika walioko Uturuki kuwasiliana na maafisa wa ubalozi wa Uganda waweze kuwasaidia kuwasiliana na jamaa zao na pia misaada midogo.
Soma pia: Juhudi zahamia kwa manusura huku vifo vya tetemeko Uturuki na Syria vyapindukia 35,000
Kulingana na takwimu, hadi sasa zaidi ya watu elfu thelathini wamshepoteza maisha yao katika janga hilo la tetemeko la ardhi lililokumba mataifa ya Uturuki na Syria.