SiasaAsia
UNHCR yahofia kutekelezwa wakimbizi wa Rohingya
17 Oktoba 2023Matangazo
Grandi amewaambia waandishi habari kandoni mwa mkutano wa kikanda unaofanyika mjini Bangkok, Thailand, kwamba msaada wa kibinaadamu unapunguwa kutokana na mizozo nchini Ethiopia, Sudan, Afghanistan, Ukraine na Israel.
Soma zaidi: Warohingya wakumbuka miaka sita ya mauaji ya halaiki
Amesisitiza kwamba mzozo wa Rohingya haupaswi kusahaulika na kama michango itapungua kutakuwa na shida.
Grandi pia amesema mzozo wa Rohingya ulikuwa na asilimia 42 ya kiwango jumla cha fedha cha milioni 875.9 zinazohitajika mwaka huu.