UN yatoa dola milioni 100 kukabiliana na matukio ya dharura
31 Agosti 2024Matangazo
Akizungumza baada ya kutangazwa kwa msaada huo jana Ijumaa, Kaimu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya kiutu Joyce Msuya amesema mataifa hayo yanakabiliwa na ukosefu wa fedha na kusababisha mashirika ya kiutu kushindwa kutoa msaada muhimu wa kuokoa maisha ya watu.
Zaidi ya theluthi moja ya ufadhili huo utaelekezwa Yemen na Ethiopia ambako watu wanakabiliwa na njaa, maradhi, majanga yanayotokana na hali ya hewa pamoja na changamoto ya watu kukosa makazi. Mataifa mengine yatakayopokea msaada huo ni pamoja na Myanmar, Mali, Burkina Faso, Haiti, Cameroon, Msumbiji, Malawi na Burundi.