UN yahofia usalama wa raia walioko Rafah
10 Februari 2024Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa antonio Guterres, Stephane Dujarric amesema kile kilicho dhahiri ni kwamba watu hao wanatakiwa kulindwa na kuongeza kuwa wasingependa kuona idadi kubwa ya watu wakilazimishwa kuyahama makaazi yao.
Zaidi ya watu milioni moja wanajihifadhi kwenye mji huo wa kusini mwa Ukanda wa Gaza wengi wakiwa wamekimbia mashambulizi ya ardhini ya Israel ya Hamas.
Soma pia: Israel yaushambulia mji wa Rafah
Hapo jana ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoratibu Misaada ya Kibinaadamu ilisema msongamano mkubwa wa watu katika mji huo utaongeza ugumu wa kuwalinda iwapo kutakuwa na operesheni ya ardhini.
Inaarifiwa kuwa hata barabara za mji huo zimezibwa kwa mahema yaliyofungwa na familia zinazotafuta eneo tambarare na safi la kuishi.