JamiiSudan Kusini
UN: Watu 700,000 waathiriwa na mafuriko Sudan Kusini
6 Septemba 2024Matangazo
OCHA limesema mafuriko yamesababisha uharibifu mkubwa kwa nyumba, mazao na miundombinu muhimu, kuvuruga mfumo wa elimu na huduma za afya na kuongeza hatari ya milipuko ya magonjwa.
Soma pia: Takriban watu 30 wauawa baada ya kuporomoka kwa bwawa, Sudan
Shirika hilo la Umoja wa Mataifa Iimesema kufikia Septemba 5, mafuriko yameathiri zaidi ya watu 710,000 katika kaunti 30 kati ya 78.
Mashirika ya misaada yameonya kuwa nchi hiyo inakabiliwa na mafuriko mabaya zaidi kuwahi kutokea katika miongo kadhaa na OCHA imesema wengi bado hawapati misaada wanayoihitaji.