UN: Ujenzi wa Gaza baada ya vita kuchukua hadi miaka 80
2 Mei 2024Matangazo
Tathmini hiyo inayolenga kutoa makadirio ya athari za kiuchumi na kijamii, imetolewa na Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP).
Lakini ripoti hiyo imesema ikiwa vifaa vya ujenzi vitatolewa kwa haraka kama ilivyokuwa wakati wa mgogoro wa mwaka 2021, basi muda huo unaweza kupungua na kushuhudia ujenzi wa Gaza ukikamilika ifikapo mwaka 2040.
Soma pia:Itachukuwa miaka 16, dola bilioni 40 kuijenga tena Gaza - UM
Vita vya Israel huko Gaza ambavyo vimedumu karibu miezi saba sasa, vimesababisha vifo vya zaidi ya watu 34,500 pamoja na uharibifu mkubwa wa mali na miundombinu.
Takwimu za mamlaka ya Palestina zinaonyesha pia kuwa karibu nyumba 80,000 zimeharibiwa.