MigogoroEthiopia
UN: Mzozo wa Ethiopia wahofiwa kuenea nchi nzima
18 Septemba 2023Matangazo
Wataalamu wa masuala ya haki wa Umoja wa Mataifa wamesema hii leo kuwa ukiukwaji mkubwa wa haki za binaadamu bado unafanywa nchini Ethiopia licha ya kuwepo makubaliano ya amani kaskazini mwa nchi hiyo.
Ukiukwaji mkubwa umeripotiwa kuongezeka maeneo ya Amhara na Oromia.
Mohamed Chande Othman, mkuu wa Tume hiyo ya wataalamu, amesema hali nchini Ethiopia ni mbaya mno na kumekuwa kukishuhudiwa vitendo vya ukatili, uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binaadamu, na wameonya kuwa mzozo huo unaenea kote nchini Ethiopia na hivyo utulivu wa ukanda huo kuwa hatarini.
Novemba mwaka jana, makubaliano ya amani kati ya serikali ya shirikisho ya Ethiopia na waasi katika eneo la Tigray yalihitimisha mzozo wa kikatili uliodumu kwa miaka miwili.