1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sheria na HakiRwanda

UN : Mfumo wa hifadhi ya wakimbizi wa Rwanda haujitoshelezi

11 Juni 2024

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia wakimbizi UNHCR limesema mfumo wa kuwahifadhi wakimbizi wa Rwanda bado haujitoshelezi.

https://p.dw.com/p/4gutb
Shirika la UNHCR limesema mfumo wa kuwahifadhi wakimbizi wa Rwanda bado haujitoshelezi
Shirika la UNHCR limesema mfumo wa kuwahifadhi wakimbizi wa Rwanda bado haujitosheleziPicha: Fathi Nasri/AFP/Getty Images

Shirika hilo limesema limepata ridhaa ya kuichagiza Mahakama Kuu ya Uingereza, kutokana na sera ya taifa hilo yenye kutaka kuwapeleka wanaotafuta hifadhi kwenye taifa hilo la Afrika Mashariki.

Wanasheria wanaomwakilisha Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Wakimbizi wanasema kuwapeleka wanaotafuta hifadhi nchini Rwanda kunawaweka katika hatari ya kuhamishiwa katika nchi nyingine ambako wanaweza kukabiliwa na mateso au hata kifo.

Awali akijibu wasiwasi huo wa kiusalama, Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak, amesema Rwanda lazima itazamwe kuwa nci nchi salama.