UN: Mamilioni ya watoto,wanawake wapo hatarini Pakistan
1 Septemba 2022Shirika linaloshughulikia masuala ya ya watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF limesema mamilioni ya watoto na wanawake wajawazito wapo hatarini katika maeneo ambayo yamekubwa na mafuriko nchini Pakistani na wanahitaji msaada wa dharura wa mahitaji muhimu.
Hadi sasa baadhi ya maeneo ambayo yameathiriwa vibaya misaada ya kiutu imeanza kusambazwa ikiwemo matibabu na kufunguliwa kwa kambi za kujihifadhi.
Ripoti ya UNICEF inaonesha kwamba watoto katika maeneoambayo mafuriko yameathiri kwa kiwango kikubwa wanakabiliwa na magonjwa ya kuambukiza, kuzama kwenye maji,utapiamlo kutokana na mafuriko ambayo yamelikumba taifa hilo la kusini mwa Asia.
mvua za kubwa zaidi za msimu inazitarajiwa kuendelea kwa wiki mbili mfululizo haikuwahi kushuhudiwa katika kipindi cha miongo mitatu na imesababisha idadi kubwa ya watu kupoteza maisha.
Soma pia:Mafuriko yawaua zaidi ya watu 1,000 huko Pakistan
Umoja wa Mataifa umesema takriban wanawake wajawazito 600,000 katika mikoa iliokumbwa na mafuriko wanauhitaji mkubwa wa huduma za matibabu na huduma ya afya ya akili.
Msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amesema kwa mujibu wa serikali ya Pakistan karibu vituo 900 vya afya vimeharibiwa na kuwaacha mamilioni ya watu bila kupata huduma za afya na matibabu.
Ameongeza tayari wameanza kushirikiana kwa ukaribu na serikali ili kufikisha huduma za kiutu katika maeneo ambayo bado hali ni mbaya.
"WHO imeongeza hatua za ufatiliani wa magonjwa ya kuhara,kipindupindu na magonjwa mengine ya kuambukiza"
Aliongeza shirika hilo limeongeza nguvu ya utolewaji wa huduma pamoja na vifaa tiba kwenye baadhi ya vituo vya afya vinavyowahudumua waathirika.
"WHO inatoa dawa muhimu na vifaa tiba kwenye vituo vya afya ambavyo vinavyotibu wahanga kwenye jamii zilizoathirika." Alisema Dujarric.
Pakistan:Idadi ya waliofariki itaongezeka
Mamlaka ya Kitaifa ya Kudhibiti Majanga nchini Pakistan imesema watu zaidi ya 1,200 wamepoteza maisha kutokana na mafuriko hayo tangu mwezi June na kati ya waliofariki watoto wanakadiriwa kufikia 384 na wanawake 231 idadi ambayo inatarajiwa kuongezeka.
Zaidi ya watu milioni 33 katika wilaya 116 kati ya 160 za pakistan zimethiriwa vibaya na mafuriko hayo na kati ya wilaya hizo tayari wilaya 72 zimetangazwa kuwa ni maeneo ya maafa.
Mamia kwa maelfu ya watu kwa sasa wanaishi bila chakula, maji safi, malazi wala dawa muhimu.
Soma pia:Mfumuko wa bei wasababisha wimbi la maandamano
Mafuriko hayo yalikumba zaidi ya ekari milioni 2 za ardhi ya kilimo, kuharibu mazao ya pamba, mpunga, tende, na mbogamboaga.
Aidha taarifa zikionesha ng'ombe 730,000 wameuwawa hadi sasa, mifugo na kilimo katika maeneo mengi ya vijiji vya Pakistan ilitumika kama chanzo cha mapato kwa watu zaidi ya milioni 8.
Maji yameharibu zaidi ya nyumba milioni moja, kilometa za barabara zaidi ya 5,000 na madaraja 243.
Waziri wa fedha Miftah Ismail alikaririwa na vyombo vya habari akisema, tayari jumuia za kimataifa zimeomba kibali cha serikali kwa ajili ya kufikisha misaada ya chakula kutoka taifa jirani la India.
Hata hivyo serikali imeonekana kusita kutokana na mahusiano mabaya baina ya mataifa hayo pamoja na fukuto la kisiasa linaloendelea nchini humo.
Wanaharakati: Mzozo wa kisiasa unachangia kusua misaada
Baadhi ya wanaharakati wanaamini mivutano ya sasa ya kisiasa inatatiza juhudi za kutolewa kwa misaada.
Imran Khan, waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo, yupo kizuizini kutokana na mzozo baina yake na serikali ya waziri mkuu wa sasa Shahbaz Sharif, ambayo imekuwa ikifungua kesidhidi ya Imran na wafuasi wake huku Khan akifanya mikutano kutafuta uungwaji mkono ili kuiondoa serikali ya shirikisho madarakani
Soma pia:Upinzani Pakistan wasema kukamatwa kwa Khan kutazusha balaa
Baadhi ya wataalam wanaamini kwamba taasisi za serikali za kudhibiti majanga hazina uwezo wa kukabiliana na uharibifu wa mafuriko kwa kiwango kikubwa.
Hata hivyo Serikali imetupilia mbali dhana kwamba haijafanya vya kutosha kuwasaidia watu.