1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiMalawi

UN: Kimbunga chasababisha watu nusu milioni kuhama Malawi

22 Machi 2023

Umoja wa Mataifa umesema zaidi ya watu nusu milioni wameyahama makazi yao kutokana na kimbunga kikali Freddy, na kuonya kuhusu kuongezeka kwa mahitaji ya kiutu.

https://p.dw.com/p/4P33j
Malawi | Zyklon Freddy
Picha: Esa Alexander/REUTERS

Eneo la kusini mwa Malawi lilikumbwa na mvua kubwa ya kiwango cha miezi sita ndani ya siku sita.

Mafuriko na maporomoko ya ardhi yasomba nyumba, barabara na madaraja. Kimbunga hicho kilisababisha vifo vya karibu watu 500 kusini mwa nchi hiyo.

Wengine 150 wamekufa katika nchi nyingine za kusini mwa Afrika tangu mwishoni mwa Febrauri kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji - IOM limesema operesheni za utafutaji na uokozi zinaendelea.

IOM imesema zaidi ya watu 1,000 wamehamishiwa maeneo salama, na zaidi ya makaazi ya dharura 500 kufunguliwa nchini Malawi.