UN: Karibu watu milioni moja wameyahama makazi yao DRC
8 Oktoba 2024Matangazo
Hayo ni kwa mujibu wa mkuu wa masuala ya haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa.Volker Turk amesema ukiukwaji wa haki za binaadamu unaongezeka na kwamba hali nchini Kongo inazidi kuwa mbaya kila uchao, huku akitaja wasiwasi wake kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu wanaosubiri kunyongwa baada ya DRC kurejesha hukumu ya kifo.Turk, ambaye aliitembelea DRC mwezi April, ameliambia Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa kwamba nchi hiyo ya Afrika ya kati inakabiliwa na ongezeko kubwa la ghasia, kuhatarisha maslahi ya kikanda na kimataifa, unyonyaji wa mashirika kadhaa na utawala dhaifu wa sheria.