1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Ulaya wakubaliana juu ya sheria muhimu ya AI

9 Desemba 2023

Nchi za EU zakubaliana kuandaa sheria za kudhibiti miundo ya akili bandia - AI, kama ya ChatGPT, baada ya masaa 36 ya majadiliano.

https://p.dw.com/p/4Zxlc
Sheria za kudhibiti miundo ya akili bandia - AI, kama ya ChatGPT, kuandaliwa na Umoja wa Ulaya
Sheria za kudhibiti miundo ya akili bandia - AI, kama ya ChatGPT, kuandaliwa na Umoja wa UlayaPicha: imago images/Imaginechina-Tuchong

Nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya pamoja na wabunge wamefikia makubaliano jana Ijumaa( 08.12.2023) juu ya namna ya kuandaa sheria za kudhibiti miundo ya akili bandia - AI, kama ya ChatGPT, baada ya masaa 36 ya majadiliano.

Kwenye mkutano uliofanyika Brussels, washiriki wa mazungumzo walikubaliana juu ya vikwazo vya jinsi AI inavyoweza kutumika Ulaya, bila ya kuathiri uvumbuzi katika sekta hiyo wala matarajio ya wataalamu wa baadaye wa AI barani Ulaya.

Wakati uwezo mkubwa wa ChatGPT katika kuandika insha na mashairi ukiashiria maendeleo ya haraka ya akili bandia, wakosoaji wana wasiwasi juu ya namna teknolojia hiyo inavyoweza kutumika vibaya.