UchumiUjerumani
EU na China ziko tayari mazungumzo kuhusu ushuru wa magari
24 Juni 2024Matangazo
Waziri wa masuala ya biashara pamoja na Waziri wa Uchumi wa Ujerumani wamesema mwishoni mwa wiki iliyopita kwamba kila upande umeonyesha utayari kuzungumzia suala hilo.
Wanasema haya wakati vyombo vya habari vya China vikisema leo kwamba Beijing inaushinikiza Umoja wa Ulaya kuachana na mipango hiyo ya kupandisha ushuru ifikapo Julai 4.
Umoja wa Ulaya ulipanga kupandisha ushuru kutoka asilimia 17.4 hadi 38.1 wa magari hayo ya umeme ya China kwa muda wa miezi minne, kuanzia Julai 4, hatua iliyochochea mzozo wa kibiashara.