UN yaonya kuhusu hatari ya kutokea magonjwa huko Gaza
30 Desemba 2023Eneo hilo ndiko walikokimbilia makumi kwa maelfu ya watu kutokana na mashambulizi ya mabomu ya Israel.
OCHA imesema watu hao wanaishi katika mazingira duni huku huduma za afya zikiwa zimeelemewa hasa kutokana na wimbi jipya la watu kuwasili eneo hilo kutokana na amri ya jeshi la Israel.
Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Tedros Adhanom Ghebreyesus , amesena kwamba kuharisha na matatizo kwenye mfumo wa kupumua ni miongoni mwa magonjwa yanayoripotiwa katika makaazi hayo.
Takriban watu 180,000 tayari wanakabiliwa na matatizo ya kupumua huku watoto zaidi ya 136,000 walio chini ya umri wa miaka mitano wakikumbwa na magonjwa ya kuharisha. Kulingana na Wizara ya Afya huko Gaza inayodhibitiwa na Hamas, mzozo huo tayari umesababisha vifo vya Wapalestina 21,672.