Israel: Tumesikitishwa na shambulizi lenye madhara Gaza
29 Desemba 2023Eylon Levy, msemaji wa serikali ya Israelamesema hilo ni kosa la kusikitisha na halikupaswa kutokea na kuongeza kuwa mkakati wao ni kupunguza vifo vya raia huku wakiwashutumu Hamas kutoheshimu hilo.
"Tunasikitika kuona watu wamepoteza maisha kwa sababu tunajaribu kufanya kila tuliwezalo ili kupunguza vifo vya raia wakati Hamas wana mkakati wa kuviongeza. Tunaendelea kujifunza na kuzidisha juhudi zetu za kuwaweka raia eneo salama." Alisema Levy.
Soma pia:Matukio yanayoendelea katika vita vya Israel-Hamas
Wizara ya Afya inayodhibitiwa na Hamas ilisema kuwa zaidi ya watu 70 waliuawa wakiwemo watoto huku maafisa wa Umoja wa Mataifa wakibaini kuwa watu 86 waliuawa.
Shambulio hilo la Desemba 24 lilifanywa kwenye kambi yaal-Maghazi wanakoishi wakimbizi wapatao 33,000.