1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel: Mapambano dhidi ya Hamas yatadumu miezi kadhaa

27 Desemba 2023

Mkuu wa majeshi ya Israel Luteni Jenerali Herzi Halevi amesema vita kati ya Israel na kundi la wanamgambo la Hamas vitaendelea kwa miezi mingi zaidi.

https://p.dw.com/p/4acE4
Israel | Mkuu wa majeshi ya Israel Luteni Jenerali Herzi Halevi
Mkuu wa majeshi ya Israel Luteni Jenerali Herzi Halevi akizungumza na wanajeshi ambao wanaendeleza oparesheni ya kijeshi katika Ukanda wa GazaPicha: IDF/UPI Photo/Newscom/picture alliance

 Ameyasema hayo wakati wanajeshi wake wakiendeleza mapambano yao ndani ya Ukanda wa Gaza ambako watu zaidi ya 20,000 wameuwawa kufuatia uhasama kati ya pande hizo mbili. 

Halevi amesema malengo ya vita hivyo ni muhimu na sio rahisi kuyafanikisha na kwahivyo vita vitaendelea kwa miezi kadhaa ijayo. 

Soma pia:Netanyahu: Vita vya Gaza vina gharama kubwa kwa Israel

Kwa upande wake msemaji wa jeshi la Israel Daniel Hagari amesema jana joni kwamba wanajeshi wengine wanaendeleza mapambano Kusini mwa Gaza mjini Khan Yunis na wametanua operesheni zao katika eneo hilo. 

Wasiwasi wa hali ya kibinaadamu kuzidi kuwa mbaya katika Ukanda waGaza umezidisha miito ya kusitishwa kwa vita vinavyooendelea huku visa vya Waasi wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran kuuingilia mzozo huo kwa kuliunga mkono kundi la Hamas vikizidisha hofu ya vita kusambaa katika maeneo mengine ya Mashariki ya Kati.