Umoja wa Mataifa waongeza muda wa kikosi cha polisi Haiti
1 Oktoba 2024Matangazo
Uamuzi huo umechukuliwa baada ya Baraza hilo la usalama kuukataa mwito uliotolewa na Haiti wa kuanzisha mazungumzo ya kukibadilisha kikosi hicho kuwa ujumbe wa kuweka amani wa Umoja wa Mataifa.
Soma zaidi: Marekani yaachana na wazo la jeshi la UM Haiti
Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Linda Thomas-Greenfield, alisema uamuzi uliopitishwa kwa kauli moja na wanachama 15 wa Baraza la Usalama unatuma ujumbe mzito kwa Haiti.
Balozi huyo alisema hatua hiyo ni juhudi za kusaidia kurudisha usalama na uthabiti katika taifa hilo.