1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Mataifa wasifu makubaliano ya Israel na Hamas

22 Novemba 2023

Umoja wa Mataifa umekaribisha makubaliano kati ya Israel na Hamas ya kuachiliwa mateka na kusitisha mapigano. Wakati huo huo Papa Francis amekutana na ndugu wa watu waliotekwa nyara na kundi la Hamas.

https://p.dw.com/p/4ZKD3
UN Secretary General Antonio Guterres
Picha: Mark J. Sullivan/Zumapress/picture alliance

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameyapokea kwa furaha makubaliano yaliyofikiwa na Israel na Hamas, upatanishi uliosimamiwa na Qatar ulioungwa mkono na Misri na Marekani.

Guterres amesema hii ni hatua muhimu iliyo katika mwelekeo sahihi. Katika taarifa yake katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa amesisitiza kuwa bado kuna mengi  yanayohitaji kufanyika.

Kufuatia kufikiwa makubaliano kati ya Israel na Hamas yakuachiwa watu waliotekwa nyara,  Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis leo amekutana na ndugu na jamaa wa mateka wa Israel waliokuwa wakishikiliwa na Hamas huko Vatican na wameelezea hisia zao baada ya Israel na Hamas kukubaliana kusitisha mapigano katika Ukanda wa Gaza kwa angalau siku nne.

Makubaliano hayo ya kusitisha mapigano yataruhusu kuingia misaada na kuachiwa mateka wasiopungua 50 waliotekwa na wanamgambo wa Hamas na wakati huo huo Wapalestina wasiopungua 150 waliozuiliwa jela nchini Israel nao wataachiliwa.

Soma:Israel na Hamas wafikia makubaliano ya kubadilishana mateka

Makubaliano hayo ya kusitisha mapigano yataruhusu kuingia misaada na kuachiwa mateka wasiopungua 50 waliotekwa na wanamgambo wa Hamas na wakati huo huo Wapalestina wasiopungua 150 waliozuiliwa jela nchini Israel nao wataachiliwa.

Kabla ya hadhira yake ya kila wiki, Papa Francis alikutana kwa wakati tofauti na ndugu na jamaa wa mateka wa Israeliwalioshikiliwa mateka na kundi la Hamas na watu wanaoishi nchini Italy walio na ndugu zao Palestina.

Ufaransa imesema ina matumaini kwamba kati ya watu watakaoachiliwa raia wake watakuwa miongoni mwa watu hao.

Mataifa ya kiarabu yasifu makubaliano ya kusitisha mapigano

Nao mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za Kiarabu wamesema wanaunga mkono makubaliano ya kusitisha mapigano kwa muda kati ya Israel na Hamas lakini wamesema makubaliano hayo yanapaswa kuongezwa muda ili yawe ni hatua ya kwanza ya kusitishwa kikamilifu kwa uhasama kati ya pande hizo mbili.

Rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas
Rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas Picha: Saudi Press Agency/Newscom/picture alliance

Rais wa Uturuki, RecepTayyip Erdogan amesema huenda akasafiri kwenda Misri hivi karibuni kujadili jinsi ya kuharakisha shughuli za kuwaondoa wagonjwa kutoka Gaza na hatua zingine.

Soma:Baraza la mawaziri la Israel laidhinisha makubaliano ya kuachiliwa kwa mateka

Kwa upande wake waziri Mkuu wa India Narendra Modi amewataka viongozi wa mataifa 20 makubwa kiuchumi duniani wafanye kila linalohitajika ili kuhakikisha mzozo kati ya Israel na Hamas haupanuki na kuwa mzozo mpana kwa sababu ukosefu wa usalama na utulivu katika eneo la Asia Magharibi unatia wasiwasi.

Modi alizungumza hayo wakati waufunguzi wa mkutano wa kilele wa mataifa wanachama wa kundi la G20 ambapo India inashikilia urais kabla ya kuipa kijiti Brazil itakayochukua uenyekiti wa G20 mwezi ujao.

Vita vilianza baada ya wanamgambo wa Hamas mnamo Oktoba 7 kuanzishamashambulio mabaya kuwahi kutokea katika historia ya Israel na kusababisha vifo vya takriban watu 1,200 wengi wao wakiwa raia, kwa mujibu wa serikali ya Israel.

Soma:Ujerumani yahimiza uwajibikaji wa kimataifa katika ukanda wa Gaza

Hamas na makundi mengine ya wapiganaji wa Kipalestina pia yaliwachukua mateka takriban Waisraeli 240 na wageni, miongoni mwao wakiwa wazee na watoto. Israel imetangaza vita dhidi ya Hamas, ikiapa kuwarejesha mateka nyumbani na kuliangamiza kundi hilo la wanamgambo.

Watu zaidi ya 500 wadaiwa kuuwawa hospitalini Gaza