1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel na Hamas wakubaliana kuachiwa mateka na wafungwa

22 Novemba 2023

Israel na Hamas leo zimetangaza makubaliano leo, ya kuachiwa kwa mateka 50 na wafungwa kadhaa wa Kipalestina, makubaliano ambayo pia yanatoa nafasi ya kusitishwa mapigano kwa siku nne katika Ukanda wa Gaza

https://p.dw.com/p/4ZIuQ
Israel | Mwanamke akitazama picha za mateka wa Israel
Israel | Mwanamke akitazama picha za mateka wa IsraelPicha: Oded Balilty/AP/picture alliance

Katika mafanikio ya kwanza makubwa ya kidiplomasia katika vita hivyo, wanamgambo wa Hamas watawaachia wanawake 50 na watoto waliotekwa wakati wa uvamizi walioufanya mnamo Oktoba 7 nchini Israel.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, baada ya mkutano wa usiku kuchaameliambia baraza lake la mawaziri kwamba ulikuwa uamuzi mgumu ila ni uamuzi sahihi.

Soma pia:Viongozi wa dunia wapongeza makubaliano ya kubadilishana mateka kati ya Istrael na kundi la Hamas

Hamas imetoa taarifa ikiukaribisha usitishwaji huo wa mapigano na kusema kwamba wapalestina 150 watawaachiwa kutoka jela za Israeli. Qatar ndiyo iliyosimamia mazungumzo hayo ya usitishwaji wa mapigano yaliyodumu kwa wiki kadhaa.