1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Afrika walaani mapinduzi yanayoteka Afrika

7 Februari 2022

Umoja wa Afrika umehitimisha mkutano wake wa kilele wa kila mwaka hapo jana kwa kulaani wimbi la matukio ya  mapinduzi ambalo limesababisha mataifa kadhaa kusimamishwa uanachama wao katika umoja huo.

https://p.dw.com/p/46ciW
Äthiopien | AU Gipfel in Addis Abeba | Mohammed Schtajjeh
Picha: Shadi Hatem/APA Images/ZUMAPRESS/picture alliance

Hali ilivyo barani Afrika imesababisha hofu kubwa, hatua ambayo maafisa wakielezea kuzorota kwa demokrasia. Kimsingi migogoro hiyo ilipata nafasi kubwa katika mkutano huo wa siku mbili, uliohudhuriwa na viuongozi kutoka katika pande tofauti za bara la Afrika.

Lakini jambo lingine ambalo lilizusha joto ni lile la uhusiano wa Umoja wa Afrika na Israel. Katika kipindi kisichopindukia majuma mawili kabla ya mkutano huo kuanza Jumamosi, Burkina Faso limekuwa taifa la nne kusimamishwa uanachama na umoja huo baada ya wanajeshi kumuondoa madarakani Rais Roch Marc Christian Kabore.

Kauli moja ya viongozi wote wa Afrika.

Äthiopien | AU Gipfel in Addis Abeba | Mohammed Schtajjeh
Viongozi wa mataifa ya AfrikaPicha: Shadi Hatem/APA Images/ZUMAPRESS/picture alliance

Kwa sasa pia Guinea, Mali na Sudan nazo zimewekwa chonjo ya umoja huo wa Afrika. Mkuu wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika, Bankole Adeoye amesema kila kiongozi wa Afrika katika mkutano huo amelaaki kitendo cha kuondolewa madarakani serikali za mataifa hayo kinyume cha katiba.

Katika mkutano wake kwa waandishi wa habari jani Jumapili Adeoye amesema hakujawahi kutokea kipindi chochote katika historia ya Afrika kwa natiafa manne kusimamishwa ndani ya umoja huo.

Hali ilivyo imevunja rekodi za matukio ya mapinduzi.

Nae mwenyekiti wa kamisheni ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat alisema hali ilivyo inaleta hisia ya Afrika imerejea katika kipindi ambacho matuko ya mapinduzi yalikuwa kama matukio ya kawaidi, na ni jambo lisilokubalika.

Lakini Umoja wa Afrika pia umelalamikiwa kwa kuchukua hatua zisizosawa katika baadhi ya matukio, likiwemo la kutoisimamisha Chad, baada ya baraza la kijeshi  kuisimamisha Chad, baada ya kifo cha kiongozi wa muda mrefu wa taifa hilo Idriss Deby Itno, kilichotokea katika uwanja wa mapambano Aprili.

Katika hatua nyingine hapo Jana, viongozi wa Afrika wameusitisha mjadata tata wa uamizi wa Faki, kuitambula Israel, kwa kuahirisha zoezi la kuupigia kura ambalo lingesababisha mgawanyiko.

Hatua ya Faki ya Julai mwaka jana ilisabaisha upingwaji mkalo na mataifa yenye ushawishi ya Umoja wa Afrika yakiwemo ya Afrika Kusini na Algeria, ambaye yalisema inaleta mkanganyiko katika sura ya Umoja wa Afrika katika taarifa za uungwaji mkono wake kwa mamlaka ya Palestina.

Tofauti na hayo mjini Addis Ababa, Rais Uhuru Kenyatta amepongeza juhudi zilizofanywa na bara la Afrika katika vita dhidi ya ugonjwa wa malaria katika miaka miwili iliyopita. Uhuru alikuwa akiwasilisha ripoti ya hatua zililizopigwa katika makabiliano ya ugonjwa huo ya ALMA ya mwaka 2021.

Chanzo: AFP0653118013