SiasaUrusi
Umoja wa Ulaya wazidi kuibinya Urusi kwa vikwazo
27 Mei 2024Matangazo
Katika taarifa, mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell amesema kifo cha Navalny ni ishara nyingine inayoonesha ukandamizaji unaofanywa na serikali ya Urusi.
Vikwazo hivyo vinawajumuisha majaji wa Urusi, waendesha mashtaka na maafisa wa idara ya mahakama ambapo iwapo wana mali zozote katika Umoja wa Ulaya basi zitafungiwa na kampuni za Ulaya hazitakiwi kuwapa fedha.
Watu hao 19 pia hawawezi kuingia wala kusafiri kupitia nchi za Umoja wa Ulaya. Kremlin imekanusha kuhusika kivyovyote vile kwa serikali ya Urusi katika kifo cha Navalny.