Ukumbusho wa Wayahudi wafunguliwa mjini Berlin
10 Mei 2005Matangazo
Berlin:
Ukumbusho wa Wayahudi waliouawa na Manazi barani Ulaya unafunguliwa leo rasmi mjini Berlin. Miongoni mwa watu mashuhuri zaidi ya 1,500 walioalikwa duniani kote kushiriki katika sherehe hizo kusini mwa Lango la Brandenburg ni Rais Horst Köhler wa Ujerumani na Kansela Gerhard Schröder. Kumbukumbu hiyo imejengwa na mchora ramani maarufu wa Kimarekani, Peter Eisenman na ina mawe maalumu 2,711 yenye urefu mbalimbali. Katikati ya mawe hayo kuna njia yenye upana wa mita moja na anayetembea katika sehemu hiyo anashikwa na hofu na kuhisi kuwa ni mpweke.