1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Ukraine:Tumerejesha maeneo yaliodhibitiwa na Urusi

Hawa Bihoga
10 Julai 2023

Ukraine imesema wanajeshi wake wameendelea kusonga mbele katika maeneo ya mashariki na kusini mwa nchi hiyo na kuashiria kuelekea kwenye maeneo yanayokaliwa na vikosi vya urusi wanaodhibiti eneo la Bakhmut.

https://p.dw.com/p/4Th45
Ukraine | Krieg | Panzerabwehrraketensystem Stugna
Picha: Roman Chop/AP Photo/picture alliance

Naibu waziri wa masuala ya Ulinzi Ukraine  Hanna Maliar  amesema, vikosi vya Kyiv vimerejesha takriban kilomita za mraba 10.2 upande wa Kusini na kilomita za mraba zingine nne upande wa mashariki mwa nchi katika juma lililopita,  baada ya makabiliano makali na vikosi vya Urusi.

Kadhalika amesema wapiganaji wa Ukraine wamechukua sehemu muhimu za kamandi karibu na Bakhmut, na kuimarisha ulinzi mkali kwenye maeneo ya kuingilia na kutokea katika jiji hilo ambalo limeshuhudia mapigano makali na umwagaji mkubwa wa damu.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amekiambia kituo cha televisheni cha Marekani cha ABC mapema leo, kabla ya kilele cha mkutano wa NATO kwamba kila siku ni hasara mpya kwa Ukraine.

"Tunachokitaka ni kusonga mbele katika kukomboa maeneo yalio chini ya udhibiti wa Moscow." Alisema Zelensky

Katika mkururo wa mashambulizi ya anga ya Urusi katika miji ya kimkakati ya Ukraine, mamalaka ya mji wa Zaporizhzhia imesema shambulizi la anga la Urusi katika shule moja kusini mwa Ukraine limewaua watu wazima wanne wakati watu walipokusanyika kupokea msaada wa kibinadamu.

Moscow ambayo mara zote imekuwa ikikanusha kulenga shabaha katika maeneo ya kiraia, imekanusha juu ya shambulio hilo.

Kupitia maafisa wake wameendelea kukanusha hadharani juu ya madai mengine ya kutekeleza uhalifu wa kivita tangu uvamizi wake mwaka uliopita.

Viongozi wa Afrika wataka kumaliza mzozo wa Ukraine

Soma pia:Ukraine yasema uwezo wa angani wa Urusi ni tatizo kubwa

Msemaji wa wizara ya Ulinzi Urusi Generali  Igor Konashenkov amsema vikosi vya Moscow, vilifanikiwa kuzima mashambulio kadhaa kutoka kwa wapiganaji wa Ukraine katika eneo la Toretsk  huko Donetsk.

"Takriban wanajeshi 275 wa Ukrene na mamluki wa kigeni walidhibitiwa," Igor alisema katika video ambayo ilioelekezwa kwa umma.

"Tanki moja na magari manne yaliharibiwa. Pia, ghala la risasi la kikosi cha 24 cha Kikosi cha Wanajeshi cha Ukraine kiliharibiwa karibu na jiji la Toretsk, Donetsk."

Kremlin: Kyiv kujiunga NATO ni hatari na kitisho kwa Urusi

Kremlin imesema leo kwamba uanachama wa Ukraine kwa NATO utakabiliwa na matokeo mabaya zaidi kwa usalama wa Ulaya ambao tayari umeharibiwa nusu yake.

Msemaji wa kremlin Dmitry Peskov ameonya kuelekea kilele cha mkutano wa NATO baadae wiki hii na kusisitiza kujiunga kwa Kyivni hatari na kitisho kwa Urusi.

Hata hivyo Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema hatarajii Ukraine kujiunga na NATO hadi baada ya mzozo huo.

Soma pia:Uturuki yaunga mkono azma ya Ukraine kujiunga na NATO

Lakini ameonekana kuelekeza matumaini yake huko Lithuania kwenye kilele cha mkutano wa NATO akisema utatoa "ishara ya wazi" kuhusu nia ya kuiingiza Ukraine katika muungano huo wa kijeshi wenye wananchama 31, hadi sasa.