1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Ukraine yadai kukomboa eneo zaidi kutoka mikononi mwa Urusi

10 Julai 2023

Ukraine imesema leo vikosi vyake vimekomboa eneo la ukubwa wa kilometa 14 za mraba upande wa mashariki na kusini mwa nchi hiyo kutoka mikononi mwa jeshi la Urusi katika cha wiki moja iliyopita.

https://p.dw.com/p/4TfLV
Ukraine | vita
Askari wa Ukraine wakisimika mfumo wa kuzuia mizinga karibu na BakhmutPicha: Roman Chop/AP Photo/picture alliance

Ukraine imesema leo vikosi vyake vimekomboa eneo la ukubwa wa kilometa 14 za mraba upande wa mashariki na kusini mwa nchi hiyo kutoka mikononi mwa jeshi la Urusi katika cha wiki moja iliyopita.  Hayo yameelezwa na msemaji wa jeshi la Ukraine Andriy Kovalyov alipozugumza na televisheni ya taifa hilo.

Soma pia: Ukraine yaanzisha mashambulizi kuyakomboa maeneo ya kusini

Afisa huyo amesema chini ya kampeni yake ya kujibu mapigo, wanajeshi wa nchi hiyo wamefanikiwa kurejesha udhibiti wa eneo la kilometa 10 za mraba huko upande wa kusini na kilometa nyingine 4  zimekombolewa kweye mji wa Bakhmut uliokuwa kitovu cha mapambano miezi ya karibuni.

Serikali mjini Kyiv imearifu kwamba kwa jumla tangu kuanza kwa operesheni yake mwezi uliopita vikosi vya Ukraine vimekomboa eneo lenye ukubwa wa kilometa 183 za mrabazilizokuwa zikishikiliwa na Urusi.