Ukraine yazishambuliwa Moscow, Crimea kwa droni
31 Julai 2023Wizara ya ulinzi ya Urusi imesema droni moja iliyoilenga Moscow ilidunguliwa katika viunga vya mji huo na nyingine mbili zikaharibiwa na kuanguka katika jengo moja la ofisi mapema jana.
Kufuatia mashambulizi hayo ya droni, Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine akaonya kuwa vita vinaielemea Urusi.
Soma: Urusi kuchukua jukumu la kusafirisha nafaka barani Afrika
Urusi yaituhumu Ukraine kufanya mashambulizi ya droni Moscow
Urusi imelengwa na mfululizo wa mashambulizi ya karibuni ya droni, ikiwemo kwenye Ikulu ya Kremlin na miji ya Urusi karibu na mpaka na Ukraine -- ambayo Moscow inasema yanafanywa na Kyiv.
Wakati huo huo, maafisa wamesema Saudi Arabia mapema mwezi Agosti itakuwa mwenyeji wa mkutano wa kilele wa amani utakaoandaliwa na Ukraine ili kutafuta njia ya kuanzisha mazungumzo kuhusu vita vya Urusi nchini mwake.
Urusi haijaalikwa katika mkutano huo.