Ukraine, Urusi zapambana vikali Kursk
6 Januari 2025Matangazo
Akitowa ripoti ya hali ya kivita jioni ya jana, Mkuu wa Majeshi wa Ukraine alisema wamerikodi matukio 42 ya mapigano kwenye mkoa huo, ambapo 12 kati yao bado yanaendelea.
Vyombo vya habari vya Urusi vimeripoti mashambulizi ya droni karibu na Kursk, ambayo vimesema yamejibiwa.
Soma zaidi: Ukraine yaanzisha mashambulizi mapya ya kijeshi Kursk
Hakuna upande ambao umezungumzia matokeo ya mapigano hayo hadi sasa.
Mwaka jana, vikosi vya Ukraine vilivuuka mpaka na kuingia kwenye mkoa huo na kufanikiwa kushikilia maeneo muhimu.
Urusi kwa upande wake imetuma wanajeshi 50,000 wakiwemo 10,000 kutoka Korea Kaskazini, na imefanikiwa kurejesha takribani nusu ya maeneo yaliyokuwa yametwaliwa na Ukraine.