1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Ukraine yaanzisha mashambulizi mapya ya kijeshi Kursk

5 Januari 2025

Ukraine imesema leo Jumapili kwamba vikosi vyake vimeanzisha mashambulizi mapya ya kijeshi katika mji wa magharibi wa Urusi wa Kursk ikiwa ni muendelezo wa mashambulizi yao ya kushtukiza katika eneo hilo.

https://p.dw.com/p/4oq0V
 Kursk- 2025 | Ukraine
Athari za shambulio la Ukraine katika mji wa KurskPicha: REUTERS

Ukraine imesema leo Jumapili kwamba vikosi vyake vimeanzisha mashambulizi mapya ya kijeshi katika mji wa magharibi wa Urusi wa Kursk ikiwa ni muendelezo wa mashambulizi yao ya kushtukiza katika eneo hilo tangu wakati wa majira ya joto mwaka jana.

Akiandika katika mtandao wa Telegram kuelezea mashambulizi hayo mapya, Mkuu wa ofisi ya rais nchini Ukraine, Andriy Yermak amesema Urusi "itakipata inachostahili" na amethibitisha katika njia isiyo ya moja kwa moja taarifa zilizochapishwa na mitandao mbalimbali juu ya mashambulizi ya Ukraine huko Kursk.

Soma zaidi.Urusi yaapa kulipiza kisasi baada ya Ukraine kufyetua makombora ya masafa marefu 

Jeshi la Ukraine lenyewe halijatoa tamko lolote kuhusu mashambulizi hayo. Kwa upande mwingine Urusi yenyewe imethibitisha kwamba Ukraine imezindua mashambulizi hayo ya kivita katika eneo hilo la mpaka la Kursk.

Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema katika taarifa kwamba vikosi vya Ukraine vimefanya mashambulio mapya ya kujaribu kuwazuia wanajeshi wa Urusi kusonga mbele katika uwanja wa mapambano huko Kursk.