SiasaIsrael
Wingu lagubika makubaliano ya amani wakati wa Ramadhan, Gaza
10 Machi 2024Matangazo
Meli ya misaada ya Uhispania iliyobeba chakula inatarajiwa kuondoka Cyprus hivi karibuni kwa ajili ya kusafirisha misaada hiyo inayolenga kupunguza mateso kwa watu wa Gaza wanaokabiliwa na vita kwa mwezi wa sita sasa.
Kundi lisilo la kiserikali la Open Arms linaloshirikiana na shirika la misaada la Marekani la World Central Kitchen, limesema meli hiyo iliyobeba tani 200 za vyakula, litavishusha katika pwani za Gaza ambako imejenga bandari ndogo.
Katikati ya hofu ya janga la njaa katika baadhi ya maeneo yaliyozingirwa ya Gaza, ndege kutoka Marekani, Jordan na kwingineko zimekuwa zikidondosha vyakula vya misaada, lakini mashirika ya Umoja wa Mataifa yameonya kwamba haviwatishi watu milioni 2.4 wa eneo hilo.