1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yatikiswa na mgomo mkubwa wa usafiri wa Umma

Hawa Bihoga
27 Machi 2023

Mamilioni ya wasafiri nchini Ujerumani leo Jumatatu wanalazimika kutafuta njia mbadala ya usafiri baada ya kushuhudiwa kwa mgomo katika sekta ya uchukuzi.

https://p.dw.com/p/4PHPD
Deutschland | Warnstreiks - Flughafen Berlin
Picha: Christian Mang/REUTERS

Mamilioni ya wasafiri nchini Ujerumani leo Jumatatu wanalazimika kutafuta njia mbadala ya usafiri baada ya kushuhudiwa kwa mgomo katika sekta  ya uchukuzi.

Viwanja vya ndege,vituo vya  mabasi na treni njia za majini kote nchini vinatazamiwa kuwa vitupu kufuatia mgomo huo unaotajwa kuwa mkubwa zaidi tangu miaka ya 1990.

Soma pia:Usafiri wa reli Ujerumani kuathirika tena siku ya Jumatatu

Katika mgomo huo utakaodumu kwa saa 24 kuanzia Jumatatu wafanyikazi milioni 2.5 wa shirikisho na manispaa, chama cha wafanyikazi Verdi na chama cha wafanyikazi wa ummadbb wanadai nyongeza ya asilimia 10.5 ya mshahara.

Treni za masafa marefu zimeahirisha safari zake,hatua iliosababisha usumbufu kwa mamilioni ya watumiaji wa huduma hiyo muhimu,hasa katika majimbo kadhaa makubwa.

msururu wa magari ya madogo yakitumika kama mbadala wa usafiri umeshuhudiwa wenye matokeo ya uchelewaji barabarani kama matokeo ya mgomo wa siku ya Jumatatu.

Wawakilishi wa Verdi na dbb wanatarajiwa kukutana tena na maafisa wa serikali leo Jumatatu kwa duru ya tatu ya mazungumzo.

Ndani ya mwezi huu pekee migomo ya hapa na pale imeshuhudiwa na kuwaathiri mamilioni ya wakaazi.