Ujerumani yasema mataifa mawili huru ndiyo suluhu pekee
22 Januari 2024Matangazo
Baerbock amesema hayo mapema hii leo (Januari 22) kabla ya kuondoka kuelekea kwenye mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya, mjini Brussels.
Amesema hata wale wanaoonyesha kutopendelea suluhu hiyo ya mataifa mawili hawajawahi luleta suluhu mbadala, huku akitoa mwito wa usitishwaji wa dharura wa mapigano katika Ukanda wa Gaza ili kuruhusu misaada ya kiutu.
Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja huo, Josep Borrel, pia amesisitiza juu ya suluhu ya mataifa mawili, na kuielezea Israel kabla ya mkutano huo kwamba haitaweza kuleta amani kwa mtutu wa bunduki.