1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Scholz ataka jamii kujizuia na chuki dhidi Wayahudi

27 Januari 2024

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz ametoa wito hii leo kwa watu kuitetea demokrasia ya Ujerumani na kupambana na chuki dhidi ya Wayahudi.

https://p.dw.com/p/4bkYA
Ujerumani I Kumbukumbu ya mauaji ya Holocaust - Berlin
Jamaa za watu waliouliwa na jeshi la Nazi wakiweka maua kwenye makaburi mjini Berlin wakati wa kumbukumbu ya miaka 79 tangu mauaji hayo ya HolocaustPicha: picture alliance/dpa

scholz amesema hayo kwenye maadhimisho ya miaka 79 ya kukombolewa kwa kambi ya mateso ya Auschwitz-Birkenau, wakati wa Vita vya Pili vya Dunia.

Kupitia ujumbe wa kila wiki wa Podcast, Scholz amesisitiza ulazima wa matukio kama hayo kutojirudia na kuirai jamii kupinga vikali visa vya chuki dhidi ya Wayahudi, ubaguzi wa rangi, unyanyasaji na kuipigania demokrasia.

Mwaka 1945, vikosi vya jeshi la Urusi viliwakomboa karibu wafungwa 7,000 kwenye kambi hiyo ya Auschwitz iliyokuwa katika eneo la Poland lililokuwa chini ya udhibiti wa Ujerumani, ambako wanajeshi wa Nazi wa Ujerumani waliwaua zaidi ya watu milioni moja, wengi wao wakiwa ni Wayahudi.