1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yakabiliwa na mgomo mwingine wa usafiri wa umma

Sylvia Mwehozi
2 Februari 2024

Ujerumani inakabiliwa na mgomo wa nchi nzima wa usafiri wa umma ulioanza leo, ukihusisha mabasi na treni za usafiri wa mijini na hivyo kutatiza mamilioni ya wasafiri.

https://p.dw.com/p/4bxQf
Waandamanaji wakiwa mbele ya bandari wakati wa mgomo wa kitaifa ulioitishwa na chama cha wafanyikazi cha Ujerumani Verde
Waandamanaji wakiwa mbele ya bandari wakati wa mgomo wa kitaifa ulioitishwa na chama cha wafanyikazi cha Ujerumani Verde Picha: Fabian Bimmer/REUTERS

Wafanyakazi wapatao elfu 90,000 wa usafiri wa umma wanafanya mgomo wa saa 24 ulioitishwa na muungano wa vyama vya wafanyakazi Verdi katika majimbo yote ya Ujerumani isipokuwa Bavaria.

Mgomo huo ni wa hivi karibuni katika wimbi la migomo iliyoikumba sekta ya uchukuzi nchini Ujerumani katika wiki za hivi karibuni.

Hapo jana kulifanyika mgomo mwingine wa wafanyakazi wa usalama katika viwanja 11 vya ndege na kuathiri abiria wapatao laki 200,000 na safari za ndege zaidi ya 1,000.

Muungano wa vyama vya wafanyakazi Verdi unadai kuboreshewa mazingira ya kazi, kupunguzwa saa za kazi na nyongeza ya siku za likizo.