1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wafanyakazi wa usalama wa viwanja vya ndege Ujerumani wagoma

Sylvia Mwehozi
1 Februari 2024

Wafanyakazi wa usalama katika viwanja vikubwa vya ndege nchini Ujerumani wanafanya mgomo wa siku moja leo katika hatua za kushikiniza nyongeza ya mishahara.

https://p.dw.com/p/4bvqQ
Köln Bonn | Chati ya ratiba za ndege
Chati ya ratiba za ndege katika kiwanja cha ndege Köln BonnPicha: Marc John/IMAGO

Mgomo huo unatarajia kutatiza maelfu ya safari za ndege za kutoka na kuingia Ujerumani.

Muungano wa vyama vya wafanyakazi wa Ver.di ambao uliitisha mgomo huo siku ya Jumanne, umewataka wafanyakazi katika viwanja 11 vya ndege Ujerumani kugoma.

Viwanja vya ndege huko Bavaria, ikiwemo kiwanja cha ndege cha Munich ambacho ni cha pili kwa ukubwa, havijaathirika na mgomo wa leo.

Soma pia:Maafisa usalama wa viwanja vya ndege waitisha mgomo Ujerumani

Safari zote za kutoka katika viwanja vya ndege vya Berlin, Hamburg na Stuttgart zilifutwa kabla ya kuanza mgomo wa leo.

Chama cha wafanyakazi wanaoendesha viwanja vya ndege cha ADV, kimekadiria kwamba takribani safari za ndege zaidi ya 1,000 zitafutwa au kucheleweshwa na abiria 200,000 wataathirika.