1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani na Kenya zasaini mkataba wa uhamiaji na ajira

14 Septemba 2024

Ujerumani na Kenya jana Ijumaa zilisaini mkataba wa ajira na uhamiaji kuruhusu wafanyakazi wenye ujuzi kutoka taifa hilo la Afrika Mashariki kuishi na kufanya kazi nchini Ujerumani.

https://p.dw.com/p/4kcTC
Ujerumani, Berlin | Ujerumani na Kenya zatia saini makubaliano ya uhamiaji
Ujerumani na Kenya zatia saini makubaliano ya uhamiajiPicha: Maja Hitij/Getty Images

Mpango huo utaisaidia Ujerumani wakati inapambana na wafanyakazi wanaozeeka na kupungua, alisema Kansela Olaf Scholz wakati akimkaribisha rais wa Kenya William Ruto mjini Berlin.

Mkataba huo pia utarahisisha urejeshwaji wa wahamiaji haramu, ingawa kuna Wakenya wachache wanaotafuta hifadhi nchini Ujerumani, ambayo inahifadhi idadi kubwa zaidi ya wahamiaji kutoka Syria na Afghanistan pamoja na wakimbizi wa vita wa Ukraine.

Kansela Scholz alisema Kenya inajivunia "idadi kubwa ya wataalam wabobezi wa TEHAMA na kuogeza kuwa wafanyakazi wake wengi wenye ujuzi na vijana wanaweza kuja Ujerumani hivi karibuni kwa kazi na mafunzo ya ufundi.

Ruto alipongeza makubaliano ya ushirikiano wa uhamiaji na wafanyakazi, ambao alisema utatumia "mtaji wa nguvukazi nchini Kenya, yenye vijana wengi.