Ujerumani kuwaondoa askari Mali kwa utaratibu
17 Juni 2023Matangazo
Msemaji wa wizara ya ulinzi ya Ujerumani amesema mjini Berlin kwamba serikali itasaidia makubaliano kati ya Umoja wa Mataifa na Mali juu ya mustakabali wa ujumbe wa amani nchini humo MINUSMA wenye wanajeshi zaidi ya 12,000 na kusisitiza kwamba Ujerumani tayari imetangaza itaondoka nchini humo Mei, 2024.
Soma pia:
Tangu kuanza kwa operesheni hiyo mwaka 2013, karibu wanajeshi 170 wa kulinda amani wameuawa na kufanya MINUSMA kuwa operesheni hatari zaidi ulimwenguni.
Waziri wa mambo ya nje wa Mali, Abdoulaye Diop jana aliliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwamba ujumbe huo unaojumuisha wanajeshi wa Ujerumani, umeshindwa na kutaka waondoke.