1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani kupanua wigo wa biashara Amerika ya Kusini

12 Machi 2023

Waziri wa Uchumi wa Ujerumani Robert Habeck ana mpango wa kupanua wigo wa makubaliano ya ukuzaji wa biashara huria kati ya Umoja wa Ulaya na Amerika ya Kusini.

https://p.dw.com/p/4OZTc
Deutschland | Habeck und Özdemir reisen nach Brasilien und Kolumbien
Picha: Britta Pedersen/dpa/picture alliance

Waziri wa Uchumi wa Ujerumani Robert Habeck ana mpango wa kupanua wigo wa makubaliano ya ukuzaji wa biashara huria kati ya Umoja wa Ulaya na Amerika ya Kusini.

Waziri huyo ameongeza kwa kusema yapo matumani ya kufikia makubaliano na kumaliza mikwamo baina ya mataifa yote mawili kwa kupitia rais wa sasa wa Brazil, Luiz Inácio Lula da Silva.

Habeck alitoa dokezo hilo jioni ya Jumamosi, kabla ya kuondoka nchini Ujerumani akiwa na waziri mwenzake wa kilimo, Cem Özdemir. Mawaziri hao wawili ni nguzo muhimu kutoka Chama Cha Kijani, "The Greens", chama cha pili kwa ukubwa katika serikali ya muungano ya Ujerumani.

Wanasafairi kwenda katika kufanikisha makubaliano ambayo kwa muda mrefu Umoja wa Ulaya umekuwa katika majadiliano na mataifa yalio kwenye muungano wa kiuchumi wa Amerika Kusini ambayo ni Brazil, Argentina, Paraguay na Uruguay.