Ujerumani kuipa NATO wanajeshi 35,000 kuanzia 2025
12 Oktoba 2023Matangazo
Shirika la habari la DPA, limesema tangazo hilo linahusisha mipango mipana iliyoandaliwa na NATO, inayoangazia ulinzi kwenye maeneo yake muhimu na hususan katika, nyakati za dharura.
Pistorius amesema karibu wanajeshi 4,000 wa Ujerumani wanatarajiwa kupelekwa na kubakia Lithuania na kutoa ndege 200 na vifaa vingine muhimu vitakavyopelekwa mara moja.
Mkakati huo unaofanyika katikati ya vita vya Urusi nchini Ukraine, unalenga kuuandaa muungano huo wa kijeshi dhidi ya matukio yoyote makubwa kama ya uvamizi dhidi ya mwanachama wa NATO, ama kutoka Urusi au kundi la kigaidi.